Monday, April 11, 2016

KLOPP ATOA MATUMAINI KWA HENDERSON KUCHEZA EURO.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema nahodha wa timu hiyo Jordan Henderson bado anaweza kuitumikia Uingereza katika michuano ya Euro 2016 pamoja na kupata majeruhi mabaya ya goti. Henderson aliumia goti katika mchezo wa Europa League ambao Liverpool walitoka sare ya bao 1-1 na Borussia Dortmund huko Ujerumani na anatarajiwa kukaa nje kwa kipindi cha wiki sita mpaka nane hivyo kumfanya kuwa na muda finyu wa kuwa fiti kabla ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 10. Lakini Klopp amesema nahodha wake huyo anaweza kurejea tena uwanjani kwa ajili ya mechi za mwisho wa msimu za Liverpool. Akihojiwa na mtandao wa klabu hiyo Klopp amesema anafahamu majeruhi aliyopata Henderson ni mabaya lakini watafanya kila wawezalo kuhakikisha anarejea hara iwezekanavyo. Uingereza inatarajiwa kupambana na Urusi, Slovakia na Wales katika kundi B huku kocha Roy Hodgson akitarajiwa kutaja kikosi chake cha mwisho Mei 12 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment