GOLIKIPA wa AS Roma, Wojciech Szczesny amesema ana matumaini Leicester City watwae ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu pamoja na kuwepo kwake katika virabu vya Arsenal. Golikipa huyo aliondoka Arsenal kwenda Roma kwa mkopo kiangazi mwaka jana baada ya ujio wa Petr Cech na amekuwa akipata nafasi katika kikosi cha kwanza toka aanze kuichezea klabu hiyo ambayo inashika nafasi ya tatu katika Serie A. Matumaini ya Arsenal kutwaa ubingwa yaliingia dosari nyingine Jumamosi iliyopita wakati walipolazimishwa sare ya mabao 3-3 na West Ham United na kuwaacha nyuma Leicester City kwa alama 13. Akihojiwa Szczesny amekiri kuwa angependa kuona Leicester wakishinda taji hilo badala ya klabu yake ya Arsenal. Golikipa huyo amesema hakuna yeyote katika soka anaweza kuelezea maajabu yanayofanywa na Leicester, hivyo pamoja na kuinga mkono Arsenal lakini angependa zaidi kuona vijana hao wa Claudio Ranieri wakishinda taji la Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment