KIPA David De Gea amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Manchester United katika kipindi cha misimu mitatu mfululizo. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania, ameonyesha umahiri wake kwa mara nyingi teana kwa kufanikiwa kuzuia wavu wake kutikiswa mara 14 kati ya mechi 32 za Ligi Kuu alizocheza mpaka sasa. De Gea anaungana na Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji mwengine wa kipekee ambaye amewahi kushinda tuzo hiyo mara tatu, ambapo nyota huyo anayekipiga Real Madrid aliwahi kutwaa mwaka 2004, 2007 na 2008. Akihojiwa katika hafla ya kumtunikia tuzo hiyo jana, De Gea amesema ni ngumu kusema chochote kwani kushinda tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo ni jambo la kipekee. De Gea aliendelea kwa kuwashukuru mashabiki wa klabu hiyo ambao anadai ndio bora kuliko wote duniani.
No comments:
Post a Comment