Tuesday, May 3, 2016

RANIERI ATAMBA BAADA YA KUTWAA TAJI LAKE LA KWANZA.

MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri amesema kutwaa taji la Ligi Kuu akiwa na timu hiyo ni fahari aliyokuwa akiisubiria kwa kipindi kirefu katika kazi yake ya ukocha. Ranieri raia wa Italia amewahi kufundisha klabu kubwa kongwe zikiwemo Juventus, Inter na Atletico Madrid lakini ni Leicester ndio hatimaye ameweza kuiongoza kushinda taji lake la kwanza kubwa. Akichukua mikoba ya Leicester kufuatia kutimuliwa kuinoa timu ya taifa ya Ugiriki, Ranieri amesisitiza amebadilika kidogo sana katika uongozi wake toka kipindi hicho mpaka kazi ya kipekee aliyofanya katika Uwanja wa King Power. Akihojiwa Ranieri mwenye umri wa miaka 64 amesema amekuwa akipambana kw akipindi kirefu lakini siku zote amekuwa na mtazamo chanya na alikuwa na mtazamo huo katika kikosi chake. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa siku zote amekuwa na mawazo kuwa siku moja atakuja kushinda taji la ligi mahali fulani na yeye ni yuleyule ambaye Ugiriki walimtimua kipindi nyuma labda kama wao watakuwa wamemsahau.

No comments:

Post a Comment