Tuesday, May 3, 2016

LAPORTE AKANUSHA TAARIFA ZA KUKUBALIANA NA MAN CITY.

BEKI wa Athletic Bilbao, Aymeric Laporte amekanusha taarifa kuwa tayari ameshafikia makubaliano na Manchester City juu ya uhamisho wake mwishoni mwa msimu huu. Taarifa za karibuni zinadai City wamekubali kutoa kitita cha euro milioni 50 kutengua mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 ikiwa ni sehemu ya mipango yao ya kuimarisha safu ya ulinzi. Hata hivyo, Laporte mwenyewe amekanusha taarifa hizo akidai kuwa haweza kuzungumza na klabu nyingine yeyote bila viongozi wake sasa kujua. Laporte ambaye mkataba wake wa sasa na Bilbao unamalizika Juni 2019, bado anaendelea kujiuguza kufuatia kuvunjika mguu wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa. Nyota huyo aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwaondoa hofu mashabiki wa Athletic kwa kukanusha taarifa hizo.

No comments:

Post a Comment