KOCHA wa timu ya taifa ya Argentina, Gerardo Martino amesisitiza Lionel Messi amekubaliana na uamuzi wa kumuacha katika kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki. Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuona itakuwa kumchosha nyota huyo wa Barcelona kucheza katika michuano yote miwili ya Olimpiki na Copa America itakayofanyika Marekani. Akihojiwa Martino amesema ameshajadiliana na Messi kuhusiana na suala hilo na wamekubaliana kuwa atashiriki michuano ya Copa Amerika pekee majira ya kiangazi badala ya kushiriki yote. Martino aliendelea kudai kuwa ni kama ilivyokuwa kwa suala la Neymar ambapo inaonekana Brazil wameamua kumtumia nyota huyo katika Olimpiki badala ya Copa Amerika.
No comments:
Post a Comment