MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Karim Benzema amekosa mazoezi leo hivyo kuongeza wasiwasi wa kuwepo katika mchezo wa nusu fainali ya marudiano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City kesho. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alitolewa nje wakati wa mapumziko katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano hiyo kufuatia kusumbuliwa na tatizo la msuli wa paja na pia aliwekwa benchi katika mchezo wa La Liga dhidi ya Real Sociedad mwishoni mwa wiki iliyopita. Wiki iliyopita meneja wa Madrid Zinedine Zidane alidai kuwa anategemea Mfaransa mwezake huyo atakuwa tayari pindi watakapokwaana na City katika uwanja wa Santiago Bernabeu, ingawa sasa suala hilo linaonekana kuwa gumu kidogo. Benzema alifanya mazoezi yap eke yake kujaribu kumuweka fiti lakini inaonekana kama nyota huyo hataweza kupona kwa wakati.
No comments:
Post a Comment