Wednesday, May 4, 2016

RANIERI ADAI VILABU TAJIRI VITAENDELEA KUTAWALA KWA MIONGO MIWILI.

MENEJA wa Leicester City amedai kuwa klabu tajiri zitatawala Ligi Kuu ya uingereza kwa kipindi cha miongo miwili ijayo kufuatia kikosi chake kutwaa taji hilo. Kikosi cha Leicester kiligharimu kiasi cha paundi milioni 57, kikiwa kikosi chenye gharama nafuu zaidi kuliko timu yeyote iliyoko nusu ya juu katika msimamo wa ligi. Akihojiwa Ranieri amesema pesa nyingi hutengeneza timu kubwa na siku zote timu kubwa hushinda karibu asilimia 99 kwa nyakati zote. Ranieri aliongeza kuwa msimu ujao utakuwa vile vile kwa timu kubwa kutawala na hata baada ya miaka 10 au 20 hali itaendelea kuwa hivyo. Taarifa zinaonyesha waliokuwa wapinzani wa karibu wa Leicester, Totteham Hotspurs walijenga kikosi chao kwa kitita cha paundi milioni 159 wakati Arsenal walitumia paundi milioni 231, Liverpool paundi milioni 260, Chelsea paundi milioni 280, Manchester United paundi milioni 395 na Manchester City paundi milioni 415.

No comments:

Post a Comment