MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simeone amesema mafanikio ya kusisimua katika mchezo wao wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich ni kama inavyokuwa katika filamu wakati inafikia mwishoni. Klabu hiyo ya Hispania ambayo ilifungwa katika hatua ya fainali chini ya meneja huyo mwaka 2014, inatarajiwa kucheza na aidha Manchester City au Real Madrid katika fainali baada ya kusonga mbele kwa bao la ugenini kufuatia sare ya mabao 2-2 waliyopata. Akihojiwa Simeone amesema katika dakika 180 walizocheza katika mechi zote mbili wameonyesha kazi waliyofanya kwa kipindi cha miaka mitatu na matumaini yake hatima hiyo inaweza kuwasaidia katika fainali. Wakiwa nyuma kwa bao 1-0 kufuatia kupoteza mchezo kwanza huko Hispania, Bayern walifanikiwa kusawazisha kwa bao lililofungwa na Xabi Alonso kwa mpira wa adhabu kabla ya kipa wa Atletico Jan Oblak hajaokoa penati ya Thomas Muller. Nyota wa Atletico Antoine Griezmann alisazisha bao hilo baa ya mapumziko kabla ya Robert Lewandowski hajaongeza lingine la pili ingawa hata hivyo halikutosha kuwavusha Bayern bapmoja na ushindi wa mabao 2-1 waliopata.
No comments:
Post a Comment