Thursday, May 5, 2016

PELLEGRINI ALALAMA KUWA HAWAKUSTAHILI KUTOLEWA.

MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesisitiza kikosi chake hakikustahili kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Real Madrid. Mabingwa hao mara 10 wa michuano hiyo walifanikiwa kutinga hatua hiyo kwa bao hilo pekee katika michezo miwili waliyokutana kufuatia shuti la Gareth Bale kumbabatiza kiungo wa City Fernandinho na kutinga wavuni jana. Katika mchezo wa jana uliofanyika katika Uwanja wa Santiago Bernabeu Madrid walishambulia lango la wapinzani wao mara 15 wakati City walifanikiwa kufanya shambulizi moja pekee la hatari katika michezo yote miwili waliyokutana. Hata hivyo, akihojiwa Pellegini amesema hakustahili kupoteza mchezo wa jana kwani bao lililofungwa na Madrid lilikuwa la bahati. Pellegrini aliendelea kudai kuwa wachezaji walicheza vyema na kwa kuwanyima Madrid muda wa kutengeneza nafasi, ila kikubwa kilichowakwamisha ni kukosa wachezaji wabunifu ambao wangeweza kuleta tofauti.

No comments:

Post a Comment