Thursday, May 5, 2016

FALCAO ATEMWA COLOMBIA.

MSHAMBULIAJI wa Chelsea Radamel Falcao ameachwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 40 cha timu ya taifa ya Colombia kilitajwa kwa ajili ya michuano maalumu ya Copa Amerika baadae majira ya kiangazi. Falcao ameanza katika mechi mbili pekee kwa Chelsea toka atue Stamford Bridge kwa mkopo wa msimu mzima kiangazi mwaka jana huku akifanikiwa kucheza mara moja pekee toka kuanza kwa mwaka huu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye ameshaifungia Colombia mabao 25 hajaitwa katika kikosi hicho toka Octoba mwaka jana wakati walipofungwa na Uruguay mabao 3-0 na aliachwa na kocha Jose Pekerman katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Bolivia na Ecuador Machi mwaka huu. Mshambuliaji wa AC Milan Carlos Bacca, Luis Muriel wa Sampdoria na Adrian Ramos wa Borussia Dortmund ni miongoni mwa washambuliaji waliojumuishwa katika kikosi hicho cha Pekerman badala ya Falcao.

No comments:

Post a Comment