Wednesday, May 4, 2016

KIPA WA CHELSEA ADAI HAENDI KOKOTE KIANGAZI.

KIPA wa Chelsea, Thibaut Courtois amekanusha uvumi kuwa anaweza kuhamia kwa mabingwa wa Ligue 1 Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu huu na kusisitiza anafuraha Stamford Bridges. Chelsea ambao kwasasa wanashikilia nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu wamekuwa na msimu mbovu na wanatarajiwa kukosa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao hivyo kuzusha tetesi kuwa wachezaji kadhaa wanaweza kuondoka. Akihojiwa Courtois amesema hajawahi kuwa na mwasiliano yeyote na PSG kwani anapenda kucheza Uingereza na anafurahia kuwepo Chelsea. Kipa huyo aliendelea kudai kuwa ana mkataba wa miaka mitatu na Chelsea hivyo ana uhakika wa asilimia 100 kuwa atabakia.

No comments:

Post a Comment