Wednesday, May 4, 2016

GUARDIOLA AMUACHIA ANCELOTTI MTIHANI.

MENEJA wa Bayern Munich, Pep Guardiola ana matumaini kuwa meneja ajaye Carlo Ancelotti ataweza kuifikisha klabu hiyo katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutolewa katika hatua ya nusu fainali na Atletico Madrid jana. Katika mchezo huo Bayern walishindi amabao 2-1 katika Uwanja wa Allianz Arena lakini ushindi huo haukutosha hivyo Atletico walisnga mbele kwa faida ya bao la ugenini ambalo lilifungwa na Antoine Griezmann katika kipindi cha pili. Vigogo hao wa Bundesliga ambao walishinda taji la michuano hiyo chini ya Jupp Heynckes mwaka 2013, wameshindwa kuvuka hatua ya nusu fainali katika misimu mitatu ambayo Guardiola amekuwa kocha. Akihojiwa Guardiola aliwapongeza Atletico kwa kufika fainali na kuongeza walijaribu kama walivyofanya hivyo dhidi ya Barcelona msimu uliopita. Guardiola aliongeza kuwa amefurahi kuifundisha Bayern na ni matumaini yake Ancelotti ataweza kuvuka hatua hiyo hiyo ya mwisho ambayo yeye ameshindwa kufanya kwa kipndi cha miaka mitatu aliyokuwa hapo.

No comments:

Post a Comment