Wednesday, May 4, 2016

MKONGWE LUCA TONI ATUNDIKA DARUGA.

MSHAMBULIAJI wa Hella Verona, Luca Toni ametangaza kuwa atastaafu soka lake rasmi mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 38 hatacheza mechi ya mwisho akiwa na Verone pale watakapokwaana na Palermo katika mchezo wa Serie A badala yake atatundika daruga zake Jumapili hii pale watakapowavaa Juventus katika Uwanja wa Bentegodi. Toni aliwaambia wana habari kuwa baada ya kufikiri kwa makini na kwa kipindi chote ambacho amekuwa katika soka ameona huu ni wakati muafaka. Mkongwe huyo aliendelea kudai kuwa wiki zi hivi karibuni zimekuwa ngumu kwake na haukuwa uamuzi rahisi kuchukua lakini anadhani wakati wake umefika sasa. Toni amewahi kung’aa na klabu za Bayern Munich na Fiorentina huku akiwahi kutwaa taji la Kombe la Dunia akiwa na Italia mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment