KIUNGO wa Manchester City, Fernandinho anaamini kikosi chao kimejifunza katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuelekea mchezo wao dhidi ya Real Madrid baadae leo. Matajiri hao wa Ligi Kuu wanapewa nafasi finyu wakielekea Santiago Bernabeu kufuatia kutoa sare ya bila kufungana na Madrid katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza uliofanyika katika Uwanja wa Etihad. Fernandinho amesema City wamekuwa wakisahihisha makosa yao ya kipidi cha nyuma ndio maana wamefanikiwa kutinga katika hatua hiyo ya nusu fainali kwa mara ya kwanza na sasa wanataka kusonga mbele zaidi. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, aliendelea kudai kuwa pamoja na kupitia magumu mengi ikiwemo suala la majeruhi na kuwakosa wachezaji wao muhimu lakini wamefanikiwa kufanya vyema kulinganisha na misimu iliyopita.
No comments:
Post a Comment