Monday, May 9, 2016

PLATINI AJIUZULU URAIS UEFA.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Michel Platini amejiuzulu wadhifa wake huo baada ya kushindwa rufani ya kupinga kufungiwa miezi sita. Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS ilitangaza kumpunguzia adhabu hiyo na sasa atatumikia kifungo cha miaka minne badala ya sita. Kufuatia uamuzi huo CAS, Platini mwenye umri wa miaka 60 aliatangza kujiuzulu nafasi yake hiyo. Platini na rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter mwaka jana walikutwa na hatia ya kuvunja kanuni za maadili kwa kufanya malipo yasiyo halali ya paundi milioni 1.3. Wawili hao ambao walikanusha tuhuma hizo, walipunguzia adhabu zake kutoka kufungiwa miaka nane hadi sita na kamati ya rufani ya FIFA kabla ya Platini hajaenda CAS kutaka kuondolewa kabisa kwa adhabu hiyo.

No comments:

Post a Comment