MSHAMBULIAJI wa Borussia Monchengladbach, Granit Xhaka amesema hakuna ofa yeyote iliyotolewa na Arsenal pamoja na tetesi zilizozagaa kuwa klabu hiyo inajiandaa kumsajili majira ya kiangazi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Emirates kwa kitita cha paundi milioni 30 baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika msimu huu unaomalizika. Lakini Xhaka mwenyewe amesema hakuna ofa yeyote iliyotolewa na klabu hiyo na kusisitiza kuwa ana furaha kuendelea kuwepo Ujerumani. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa bado ana mkataba na Gladbach mpaka mwaka 2020 hivyo ni mategemeo yake ataendelea kuitumikia klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment