Thursday, June 9, 2016

ADIDAS WAOMBA RADHI KWA KUKOSEA JINA LA COLOMBIA.

KAMPUNI ya vifaa vya michezo ya Adidas imeomba radhi kwa kuandika vibaya jina la Colombia katika matangazo yake yanayohusu jezi mpya wanazotumia timu ya taifa ya nchi hiyo katika michuano ya Copa America. Tangazo hilo ambalo linawaonyesha wachezaji wa Colombia wakiwa katika jezi nyeupe liliondolewa baada ya mitandao ya kijamii kushambulia kwa kwa kuliandika vibaya jina la nchi hiyo ambap waliandika Columbia badala ya Colombia. Katika taarifa yake kampuni hiyo yenye makao yake makuu huko Portland, Oregon imedai kuwa wanathamini ushirikiano wao na Shirikisho la Soka la Colombia na kuwaomba radhi kwa makosa hayo yaliyofanyika. Adidas wamekuwa wakitengeneza sare za Colombia toka mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment