NYOTA wa mpira wa kikapu Lebron James amefanikiwa kufunga alama 32 wakati Cleveland Cavaliers wakiwafunga mabingwa watetezi Golden State Warriors kwa vikapu 120-90 katika mchezo wa tatu wa fainali ya NBA. Baada ya kufungwa katika mechi mbili za mwanzo, Cavaliers sasa wako nyuma kwa 2-1 kati ya fainali saba ambazo zitachezwa. Kyrie Irving aliongeza alama zingine 30 kwa Cavaliers waliokuwa nyumbani huku Steph Curry akifunga alama 19 kwa Warriors. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, kocha wa Warriors, Steve Kerr amesema hawakuwa tayari kucheza hivyo wapinzani ni kama wamewapiga ngumu mdomoni. Cleveland ambao pia watakuwa nyumbani katika mchezo wa nne wa fainali Ijumaa hii, walifungwa Warriors katika fainali za mwaka jana.
No comments:
Post a Comment