Thursday, June 9, 2016

POGBA ATAMANI KUWA KAMA KINA PELE NA MARADONA.

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba amesisitiza kuwa anataka kukumbukwa kama ilivyo kwa nguli wengine kama Diego Maradona wa Argentina na Pele wa Brazil. Kiungo wa anayekipiga Juventus, amesema amepania kufikia malengo yake hayo kwa kujituma na kuhakikisha kila siku anaimarika. Pogba ameimarika na kuja kuwa mmoja kati ya wachezaji bora kabisa kwasasa toka aondoka United kuelekea Turin mwaka 2012 ambapo ameisaidia Juventus kunyakuwa mataji manne mfululizo ya Serie A na kufika fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2015. Akihojiwa na luninga ya ESPN, Pogba amesema kwasasa hadhani kama ameshafanya lolote katika soka kwani bado kuna mataji mengi hajawahi kushinda kama Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia na hata Euro. Pogba mwenye umri wa miaka 23 aliendelea kudai kuwa malengo yake ni kuendelea kuimarika na kuhakikisha anashinda kila kitu.

No comments:

Post a Comment