Thursday, June 9, 2016

MAJERUHI YAMLAZIMISHA AGGER KUTUNDIKA DARUGA MAPEMA.

BEKI wa zamani wa Liberpool, Daniel Agger amestaafu rasmi soka lake akiw ana umri wa miaka 31. Agger ambaye amekuwa akisumbuliwa kwa kipindi kirefu cha soka lake la majeruhi aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuelezea uamuzi wake huo. Agger aliandika katika twitter akiwashukuru wale wote waliomuunga mkono katika kipindi chote na kuongeza japo ni uamuzi mgumu lakini anadhani ni sahihi kwa afya yake. Beki huyo wa kimataifa wa Denmark ambaye aliondoka Liverpool mwaka 2014 baada ya kuitumikia kwa miaka nane na kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Brondby, amewahi kuichezea nchi hiyo mechi 75.

No comments:

Post a Comment