Thursday, June 9, 2016

RONALDO AIPA NAFASI ITALIA KUTWAA EURO 2016.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo ameitaja Italia kama moja ya timu ambazo zinaweza kutwaa taji la michuano ya Euro 2016. Hatua hiyo inaweza kuwa ya kushangaza haswa kutokana na mara kadhaa Italia kutopewa nafasi kutokana na kukosa nyota wenye ubora katika kikosi chao. Italia inaingia katika michuano hiyo ikiwa bila ya viungo wake mahiri Marco Verratti na Claudio Marchisio ambao wameachwa kutokana na kuwa majeruhi. Hata hivyo, Ronaldo anaamini Italia ambao hawajafungwa katika mechi zao za kufuzu michuano hiyo, ni moja timu zenye nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo sambamba na Ufaransa, Ujerumani na Italia. Ureno imepangwa katika kundi F katika michuano hiyo sambamba na Iceland, Austria na Hungary.

No comments:

Post a Comment