Friday, June 17, 2016

BALOTELLI NJIANI KWENDA UTURUKI.

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mario Balotelli anaweza kuuzwa Besiktas kama wakala wake akifanikiwa kukamilisha dili na klabu hiyo ya Uturuki. Nyota huyo wa kimataifa wa Italia msimu uliopita alicheza kwa mkopo AC Milan na wakala wake Mino Raiola alishaambiwa mapema Februari mwaka huu kumtafutia timu nyingine majira ya kiangazi mteja wake. Baada ya kuangalia uwezekano w kwenda China, Uturuki sasa inaonekana ndio mahali atakapoelekea mshambuliaji huyo aliyefunga mabao manne katika mechi 28 za mashindano yote alizoichezea Milan msimu uliopita. Akihojiwa Raiola amesema amewapa ofa Besiktas ya kumchukua Balotteli na sasa anasubiri majibu kutoka klabu hiyo. Wakala huyo aliongeza kuwa na uhakika usajili huo utafanyika kwakuwa rais wa Besiktas aliwahi kumuhakikishia huko nyuma kuwa watafanya kila wawezalo kumsajili.

No comments:

Post a Comment