Friday, June 17, 2016

SHABIKI MWINGINE WA IRELAND KASKAZINI AFARIKI DUNIA.

SHABIKI mmoja wa Ireland ya Kaskazini amefariki dunia katika Uwanja wa Lyon wakati akiishuhudia timu yake ikiichapa Ukraine katika michuano ya Ulaya inayoendelea nchini Ufaransa. Robert Rainey anayejulikana kama Archie, anadaiwa kuwa alipata shinikizo la moyo katika moja ya majukwaa ya uwanja huo. Watoa huduma ya kwanza walijitahidi kumuhudumia shabiki huyo mnene mwenye umri wa miaka 62 ndani ya uwanja huo lakini baadae alitangazwa kufariki dunia. Taarifa kutoka wa familia yake zimedai kuwa mpendwa wao huo amefariki amefariki akiwa anafanya kile anachokipenda zaidi. Huyu anakuwa shabiki wa pili wa nchi hiyo kufariki nchini Ufaransa baada ya kijana Darren Rodgers mwenye umri wa miaka 24 kufariki dunia baada ya kuangukwa kaika mwamba wa fukwe huko jijini Nice mepama wiki hii.

No comments:

Post a Comment