MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu, Steph Curry alijikuta akitolewa uwanjani kwa kosa la kurusha kikinga mdomo kwa mashabiki wakati Cleveland Cavaliers walipofanikiwa kuichapa Golden State Warriors kwa vikapu 115-101 na kupelekea fainali za NBA mwaka huu kuamuliwa na mchezo wa saba. Baada ya kucheza faulo dakika za mwishoni katika robo ya nne ya mchezo huo, Curry alionyeshwa kuchukizwa na kurusha kikinga mdomo chake ambacho kwa bahati mbaya kilimpiga shabiki aliyekuwepo pembeni.
![]() |
Mwanamuziki mkongwe Jay Z akiwa na mkewe Beyonce katika Uwanja wa Q Arena wakifuatilia mchezo huo. |
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 aliomba radhi kwa shabiki huyo kabla ya kuondoka uwanjani huko Cleveland. Kama wakipata ushindi huko Oakland Jumatatu, Cavaliers itakuwa timu ya kwanza kushinda fainali hizo huku wakiwa wametoka kwa kufungwa 3-1. Pia litakuwa taji lao la kwanza la NBA. Nyota wa Cavaliers Lebron James alifunga alama 41 na Kyrie Irving akiongeza zingine 23 katika Uwanja wao wa Q Arena, mchezo ambao ulihudhuriwa na watu mashuhuri mbalimbali akiwemo mwanamuziki mkongwe Jay Z pamoja na mkewe Beyonce.
No comments:
Post a Comment