Friday, June 17, 2016

COPA AMERICA 2016: MAREKANI YAFUZU NUSU FAINALI KWA MARA YA KWANZA TOKA 1995.



TIMU ya taifa ya Marekani imefanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza toka mwaka 1995 hatua ya nusu fainali ya michuano ya Copa America baada ya kuichabanga Ecuador kwa mabao 2-1. Mabao ya Clint Dempsey na Gyasi Zardes waliyofunga katika kila kipindi yalitosha kuwadidimiza wapinzani wao katika mchezo huo uliofanyika huko Seattle huku bao la kufutia machozi la Ecuador likiwekwa kimiani na Michael Arroyo. Akijojiwa mara baada ya mchezo huo, kocha wa Marekani Jurgen Klinsmann amesema wametokea mbali na sasa wana uchu zaidi wa kutinga hatua inayofuata. Marekani sasa wanasubiri kucheza mshindi kati ya Argentina au Venezuela katika hatua hiyo kwenye mchezo utakaofanyika jijini Houston Jumanne ijayo.

No comments:

Post a Comment