KLABU ya Medeama ya Ghana inaamini inaweza kuvuka vikwazo vya kiuchumi vinavyowakabili hivi na kwenda kuifunga TP Mazembe huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC mwishoni mwa wiki hii wakati mechi za hatua ya makundi za michuano ya Kombe la Shirikisho zitakapoanza. Klabu hiyo imekuwa ikipitisha bakuli kutafuta nauli ya kuwapeleka DRC kwa ajili ya mchezo huo huku wakiwa hawajawahi kushinda taji la michuano hiyo wakati wenzao Mazembe wakiwa tayari na mataji tisa. Rais wa Medeama Moses Armah amesema wamejiandaa kimwili na kiakili kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mazembe. Hata hivyo Armah amesema tatizo kubwa linalowakabili kwasasa ni fedha za safari yao hiyo akidai ni tatizo linaloziabili klabu nyingi zinazoshiriki michuano hiyo. Medeama ni lazima wasafiri kwenda DRC, Algeria na Tanzania ambako watakuwa kucheza na Yanga katika hatua ya makundi na kama hata kama wakimaliza mkiani mwa kundi lao wana uhakika wa kukunja kitita cha dola 150,000.
No comments:
Post a Comment