Friday, June 17, 2016

KLABU TATU ZIKO TAYARI KUTENGUA MKATABA WA NEYMAR BARCELONA - WAKALA.

WAKALA wa Neymar, Wagner Ribeiro amesema mteja wake anafuatiliwa na klabu tatu ambazo ziko tayari kutoa ofa ya euro milioni 190 ili kutengua mkataba wake Barcelona. Nahodha huyo wa Brazil alitua Camp Nou akitokea Santos mwaka 2013 na amebakisha misimu miwili katika mkataba wake wa miaka mitano aliosaini. Mazungumzo juu ya mkataba mpya bado yanaendelea huku tetesi za kuwindwa na Paris Saint-Germain, Manchester United na Real Madrid zikiendelea kuzagaa. Wakati Ribeiro akisisitiza kuwa Neymar ana furahia kuwepo Barcelona, wakal huyo amedai timu tatu zimeonyesha kuwa tayari kufikia dau la euro milioni 190 ili kutengua mkataba wake. Akihojiwa Ribeiro amesema kuna klabu tatu kubwa duniani ambazo zinataka kumsajili na kwa kuilipa Barcelona euro 190 kwa ajili ya kutengua mkataba wake.

No comments:

Post a Comment