Friday, June 17, 2016

EURO 2016: ITALIA YATINGA 16 BORA KWA KUICHAPA SWEDEN.

TIMU ya taifa ya Italia imefanikiwa kutinga hatua ya timu 16 bora katika michuano ya Ulaya inayoendelea nchini Ufaransa baada ya kuichapa Sweden kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Halmashauri uliopo huko Toulouse. Bao pekee katika mchezo huo mgumu liliwekwa kimiani na mshambuliaji wao nyota Eder katika dakika ya 88. Ushindi huo sasa unaifanya Italia kuongoza kundi E kwa alama sita wakifuatiwa na Ireland wenye alama moja ambao watacheza mchezo wao pili dhidi ya Ubelgiji wanaoburuza mkia kwenye kundi hilo. Mechi za mwisho za kundi E zinatarajiwa kuchezwa Juni 22 ambapo Italia itacheza Ireland huku Ubelgiji wakipambana na Sweden.

No comments:

Post a Comment