KLABU ya Bayern Munich imemruhu kiungo wao Douglas Costa kwenda kushiriki michuano ya Olimpiki akiwa na Brazil, hivyo kumfanya kuungana na Neymar kuwa mmoja wa wachezaji watakaokuwa wamezidi umri katika michuano hiyo. Mkurugenzi wa Ufundi wa Brazil Gilmar Rinaldi alitangaza taarifa hizo katika mkutano wa wanahabari jana muda mfupi baada ya kutimuliwa pamoja na kocha mkuu Dunga kufuatia kutolewa mapema katika michuano ya Copa America. Neymar hakushiriki michuano hiyo kwasababu Brazil iliamua kumtumia katika michuano ya Olimpiki badala yake. Costa mwenye umri wa miaka 25, alikakariwa na luninga moja mapema wiki hii akidai kuwa hadhani kama Bayern watamzuia kucheza michuano ya Olimpiki baada ya kutolewa katika michuano ya Copa America kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya misuli. Timu ambazo zitashiriki michuano ya Olimpiki, zitaruhusiwa kutumia wachezaji watatu pekee waliozidi umri wa miaka 23 katika vikosi vyao na Neymar na Costa watabakisha nafasi moja pekee kujazwa katika kikosi cha Brazil.
No comments:
Post a Comment