MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ubelgiji, Christian Benteke amesema anataka kubakia Liverpool lakini amekiri anaweza kuangalia mahali pengine kama hatakuwepo katika mipango ijayoa ya Jurgen Klopp. Benteke alijiunga na Liverpool akitokea Aston Villa kwa kitita cha paundi milioni 32.5 kiangazi mwaka jana, akisaini mkataba wa miaka mitano lakini amekuwa akishindwa kuonyesha cheche zake Anfield. Nyota huyo bado anapenda kuendelea kubakia hapo lakini kama atakuwa nje ya mipango ya Klopp anaweza kuangalia mahali pengine atakapoweza kupata nafasi ya kucheza. Akihojiwa Benteke amesema akiwa na umri wa miaka 25 sasa sio kwamba ni mkubwa sana au mdogo lakini muhimu ni kupata muda mwingi wa kucheza.
No comments:
Post a Comment