Thursday, June 23, 2016

COPA AMERICA 2016: FAINALI NI CHILE VS ARGENTINA.



MABINGWA watetezi Chile wanatarajiwa kupambana na Argentina katika fainali ya michuano ya Copa America Jumapili hii baada ya kuiangamiza Colombia kwa mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa mapema leo ambao ulilazimika kuchelewa kwa saa mbili kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha. Chile walikuwa wakiongoza kwa mabao mawili baada ya mapumziko lakini kipindi cha pili cha mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Soldier Field jijini Chicago, kilikumbwa na mvua hiyo ikabidi wazsubiri mpaka ilipokatika. Mabao ya Chile katika mchezo huo yalifungwa na Charles Aranguiz na Jose Pedro Fuenzalida aliyefunga la pili na kuzamisha jahazi la Colombia. Fainali hiyo ni kama marudio ya ile ya mwaka jana ambayo Chile waliokuwa wenyeji walishinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Colombia sasa watachuana na wenyeji Marekani katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu Jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment