Wednesday, June 1, 2016

IBRAHIMOVIC AITOLEA MBAVUNI MARMO.

MSHAMBULIAJI nyota anayewindwa na Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amekanusha tetesi za kurejea Marmo, akisisitiza kuwa kiwango chake sio cha kucheza katika Ligi Kuu ya Sweden. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 ambaye kwasasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Paris Saint-Germain kumalizika amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda United na China. Ibrahimovic aliwaambia wanahabari leo kuwa atabainisha klabu atakayokwenda pindi atakapochoka kusoma tetesi nyingi zilizozagaa. Mkongwe huyo aliwahi kuichezea Malmo ikiwa ndio klabu yake ya kwanza kuanzia mwaka 1996 mpaka 2004. Baadae akaenda kuzichezea klabu za Ajax Amsterdam, Juventus, Inter Milan, Barcelona na AC Milan kabla ya kujiunga na PSG mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment