Wednesday, June 1, 2016

BOATENG AMSHUKURU KANSELA MARKEL.

BEKI wa kimataifa wa Ujerumani, Jerome Boateng amedai kuwa ubaguzi nchini humo bado upo kwa kiasi kikubwa lakini alishukuru Kansela Angela Merkel kwa kuponda vikali kauli iliyotolewa na mwasiasa Alexander Gauland hivi karibuni. Gauland alikaririwa mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa hangependa kuwa rafiki au hata jirani na nyota huyo wa Bayern Munich ambaye ana asili Ghana. Kauli hiyo ilizua mjadala mkubwa huku ikipondwa vikali na watu mbalimbali akiwemo ofisa mkuu wa Ligi ya Soka ya Ujerumani-DFL aliyedai kuwa kauli hiyo mbaya na isiyovumilika. Naye msemaji wa Merkel amesema kansela huyo amsikitishwa sana na kauli hiyo haswa ikizingatiwa kuwa imetoka kwa mwasiasa anayeheshimika. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Boateng amesema amefarijika kuona watu mbalimbali wanavyopingana na kauli hiyo akiwemo Merkel na kuongeza kuwa vita vya kupambana na ubaguzi wa rangi bao haijaisha.

No comments:

Post a Comment