Monday, June 13, 2016
KAMA ULIMISS BAO LA MKONO LILILOITOA BRAZIL COPA AMERICA.
KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Dunga amesema hana hofu yeyote kuhusu kibarua chake baada ya kikosi chake kuenguliwa katika michuano ya Copa America na kusisitiza kuwa anahofia kifo peke yake. Brazil ilichapwa bao 1-0 na Peru na kuondolewa katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza kwa karibu kipindi cha miaka 30. Lakini mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia walilalamika kuwa bado la ushindi lililofungwa na Raul Ruidiaz katika dakika ta 75 katika Uwanja wa Foxborough huko Massachusetts lilikuwa la mkono. Akihojiwa Dunga amesema kuwa kila mtu ameona wazi kuwa bao lile lilikuwa la mkono na halikuwa halali. Wachezaji wa Brazil walijaribu kumlalamikia mwamuzi wa Uruguay Andres Cunha lakini aliamua kusimamia uamuzi wake baada ya kupata ushauri kutoka kwa msaidizi wake wa pembeni. Matokeo hao yanaifanya Brazil kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi B, nyuma ya Peru na Ecuador, ambao wote wamefuzu hatua ya robo fainali. Peru sasa wnatarajiwa kucheza na Colombia, wakati Ecuador wakiivaa Marekani ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment