KLABU ya Everton imethibitisha uteuzi wa meneja wa Southampton Ronald Koeman kuwa meneja wao mpya. Meneja huyo raia wa Uholanzi amesaini mkataba wa miaka mitatu na Everton baada ya kuondoka Southampton akiwa ameitumikia kwa miaka miwili. Akiwa amejiunga na Southampton mwaka 2014, Koeman aliiongoza kumaliza katika nafasi ya saba katika msimu wake wa kwanza kabla ya kufanikiwa zaidi na kumaliza nafasi ya sita msimu huu na kufuzu michuano ya Europa League. Koeman sasa anachukua nafasi ya Roberto Martinez ambaye alitimuliwa Mei mwaka huu baada ya kuifanya Everton kumaliza katika nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa ni nafasi yao mbovu katika historia yao. Akihojiwa Koeman amesema anaamini katika klabu, timu, mashabiki na uwez wao wa kupata mafanikio katika siku zijazo.
No comments:
Post a Comment