Tuesday, June 14, 2016

URUSI KUONDOLEWA EURO 2016.

URUSI huenda ikaenguliwa kushiriki michuano ya Euro 2016 kama mashabiki wake wakiendeleza vurugu katika mechi zao zilizobakia. Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA limeipa Urusi adhabu na pia faini ya euro 150,000 kwa vurugu za mashabiki wake walizozionyesha katika mchezo dhidi ya Uingereza uliofanyika huko Marseille. Urusi pia imeshitakiwa na kwa mashabiki wake kuonyesha vitendo vya kibaguzi na kuwasha miwako wakati wa mechi. Kundi la mashabiki wa urusi wameondolewa nchini Ufaransa baada ya matukio ya vurugu kujirudia katika michuano ya Ulaya inayoendelea. Adhabu hiyo ya kuondolewa mashidanoni itatekelezwa pale tu ambao matukio kama hayo ya vurugu yatajirudia tena. Pamoja na kupewa ruhusa ya kukata rufani kupinga adhabu hiyo, lakini waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko amesema kuwa hawatafanya hivyo.

No comments:

Post a Comment