KLABU ya Liverpool, inatarajia kuacha rasmi Kolo Toure kutokana na beki huyo kutopewa ofa ya mkataba mpya. Mkataba wa beki wa huyo unatarajiwa kumalizika kipindi hiki cha kiangazi na jina lake litakuwa miongoni katika orodha ya wachezaji watakaoachwa. Toure mwenye umri wa miaka 35 alichukuliwa kutoka Manchester City kwa uhamisho huru Julai mwaka 2013 ni mmoja kati ya wachezaji wenye ushawishi mkubwa katika klabu hiyo. Beki huyo amejizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa wachezaji wenzake na baadhi ya wafanyakazi wa klabu hiyo kutokana na uzoefu wake mkubwa alionao.
No comments:
Post a Comment