Sunday, June 19, 2016
MESSI AFIKIA REKODI YA BATISTUTA.
MSHAMBULIAJI nyota wa Argentina, Lionel Messi amefanikiwa kufikia rekodi ya mabao 54 ya mechi za kimataifa wakati walipofanikiwa kushinda mabao 4-1 na kutinga nusu fainali ya michuano ya Copa America. Bao la nne alilofunga Messi katika mchezo huo limemfanya kufikia rekodi hiyo iliyowekwa na nguli wa zamani wa nchi hiyo Gabriel Batistuta. Nyota huyo wa Barcelona, mwenye umri wa miaka 28, pia alitengeneza mabao mengine yaliyofungwa na Gonzalo Higuain mara mbili na Erik Lamela na sasa wanatarajiwa kukwaana na wenyeji Marekani katika hatua inayofuata. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Messi amesema kuwepo katika nusu fainali nyingine ya michuano mikubwa kama hiyo ni mafanikio makubwa kwao. Messi aliongeza kuwa wamefurahi kufikia hapo na pia ni jambo jema kufikia rekodi ya Batistuta lakini siku zote jambo muhimu kwake ni matokeo na sio mafanikio binafsi. Mabingwa watetezi wa taji hilo Chile wao watachuana na Colombia kwenye nusu fainali baada ya kuitandika bila huruma Mexico kwa mabao 7-0.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment