Sunday, June 19, 2016

RISICKY CHALI CHA MENDE.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech, Tomas Risicky anatarajiwa kukosa mechi zote zilizosalia za michuano ya Ulaya kufuatia kupata majeruhi ya nyonga. Kiungo huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 35, alipata majeruhi hayo katika mchezo wa Ijumaa iliyopita waliopata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Croatia na madaktari wa timu hiyo wamesema hataweza kucheza tena mechi zilizosali nchini Ufaransa. Jamhuri ya Czech wanatarajiwa kucheza na Uturuki Jumanne ijayo na ushindi kwenye mchezo huo utaweza kuwahakikishia nafasi ya kucheza hatua ya mtoano. Ili hilo liwezekane, Croatia nao watatakiwa wapoteze mchezo wao wa mwisho dhidi ya vinara wa kundi D Hispania. Hata hivyo, nafasi ya tatu inaweza kuwa nzuri kwa Czech kuvuka hatua inayofuata.

No comments:

Post a Comment