Sunday, June 19, 2016

EURO 2016 KUAMUA HATMA YA HODGSON.

MWENYEKITI wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA, Greg Dyke amesema mkataba wa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Roy Hodgson utaongezwa pale tu timu hiyo itakapofanya vyema katika michuano Ulaya inayoendelea nchini Ufaransa. Uingereza itakabiliana na Slovakia kesho wakifahamu fika kuwa ushindi utawahakikishia nafasi ya kutinga hatua ya mtoano ya michuano hiyo. Mkataba wa Hodgson unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na kocha huyo ameonyesha dalili kuwa angependa kuendelea kuinoa timu hiyo mpaka katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018. Akihojiwa Dyke amesema ni wazi kuwa kama wakitinga hatua ya nusu fainali ni mafanikio lakini kama wakitolewa katika hatua za awali majadiliano itabidi yafanyike ili kuona wapi walipojikwaa. Hodgson mwenye umri wa miaka 69, amesema FA wamekuwa wazi kwake kuwa watato uamuzi wao juu mustakabali wake baada ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment