WACHEZAJI Chile na mashabiki wao wamelazimika kushindana na sauti ya muziki wa rapa Pitbull, wakati wimbo wake ulipochezwa mwishoni wakati wakimalizia wimbo wao wa taifa kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa Copa America dhidi ya Argentina. Hiyo inakuwa mara ya pili katika kipindi cha siku mbili kwa wimbo wa taifa wa nchi kuchanganywa katika michuano hiyo. Waandaji tayari walishaomba msamaha kwa kucheza wimbo wa taifa wa Chile badala ya ule wa Uruguay kabla ya mchezo wao dhidi ya Mexico Jumapili iliyopita. Mashabiki na wachezaji wa Chile walikuwa bado wakiimba wimbo wao wa taifa wakati wimbo wa Pitbull ulipoingilia mwishoni na taarifa zinadai kuwa wimbo wa mwanamuziki huyo ndio ulikuwa ukifuatia katika orodha katika Uwanja huo uliopo Santa Clara, California. Pitbull ni mwamuziki wa Marekani aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa kuuza zaidi ya nakala milioni 60 za muziki wake na kumfanya kuongoza kwa jina la utani la Mr Worldwide.
No comments:
Post a Comment