KOCHA wa timu ya taifa ya Argentina, Gerardo Martino amedai kuwa Lionel Messi atakuwa tayari kukitumikia kikosi cha nchi hiyo katika kipindi cha siku nne zijazo. Akihojiwa mara baada ya ushindi wa mabao 2-1 waliopata dhidi ya Chile katika mchezo wao wa kwanza, Martino alielezea maendeleo ya afya ya Messi na kudai kuwa anaweza kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Panama Juni 10 mwaka huu. Argentina ambao ni mabingwa mara 14 katika michuano hiyo, walifanya kazi nzuri bila Messi katika Uwanja wa Levi. Martino aliendelea kudai kuwa katika kipindi cha siku nne Messi atakuwa fiti kwa ajili ya kucheza lakini bado wanafutilia maendeleo yake kwa karibu.
No comments:
Post a Comment