MKURUGENZI wa michezo wa Wolfsburg, Klaus Allofs amethibitisha klabu hiyo iko katika mchakato wa kumsajili nyota wa kimataifa wa Uholanzi, Vincent Janssen lakini amekiri kuwa wanakabiliwa na ushindani mkubwa katika mbio zao hizo za kumuwania mshambuliaji huyo wa AZ. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, alikuwa katika kikosi kizuri msimu uliopita akiwa mefunga mabao 27 katika mechi 34 za ligi alizocheza na kumfanya kuw amfungaji bora. Ubora huo wa hali ya juu alioonyesha umepelekea klabu nyingi kummezea mate zikiwemo Tottenham Hotspurs na Everton. Akihojiwa Allofs amesema tayari wameshaanza mazungumzo na Janssen lakini wao sio pekee wanaowania saini ya mshambuliaji huyo.
No comments:
Post a Comment