Thursday, June 16, 2016

ARDA TURAN AKIRI KUCHEZA CHINI YA KIWANGO.

KIUNGO wa kimataifa wa Uturuki, Arda Turan anadhani hakustahili kukosolewa sana pamoja na kucheza chini ya kiwango katika mchezo wao wa ufunguzi wa michuano ya Ulaya huku akiwa na matumaini ya kupata alama katika mchezo wao dhidi ya Hispania Ijumaa hii. Nahodha huyo wa Uturuki amekuwa akikosolewa vikali kwa kucheza chini ya kiwango baada ya kufungwa bao 1-0 na Croatia katika mchezo wao wa ufunguzi. Nyota huyo wa Barcelona amekiri kuwa hakuwa katika kiwango chake bora katika mchezo huo wa ufunguzi wa kundi D lakini amedai kuwa siku zote hujitoa kwa kila kitu kwa nchi yake. Akihojiwa Turan amesema pamoja na kuwa hakucheza vyema watu wanapaswa waelewe kuwa mambo hayo hutokea haswa katika soka, hivyo atajitahidi ili aweze kufanya vyema katika mchezo wao ujao.

No comments:

Post a Comment