KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low ameomba radhi baada ya picha za video kumnasa akiingiza mkono wake ndani ya suruali yake na kasha kunusa vidole vyake. Video hiyo iliyonaswa wakati wa mchezo wa michuano ya Ulaya dhidi ya Ukraine, ilisambazwa katika mitandao ya kijamii. Akihojiwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 56, ilikuwa katika hali ya shinikizo kutokana na mchezo ulivyokuwa ukiendelea hata hivyo atajaribu kubadilika siku zijazo. Low aliendelea kudai kuwa ameoziona picha hizo za video na muda mwingine mtu anaweza kufanya jambo bila kujijua hivyo anaomba radhi. Mshambuliaji wa Ujerumani Lukas Podolki pia alimtetea kocha huyo na kudai kuwa tukio hilo halijaathiri chochote kambi yao.
No comments:
Post a Comment