KLABU ya Sunderland imethibitisha kuwa kocha wake sam Allardyce amefanya mazungumzo na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kuhusu nafasi ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo. Roy Hodgson alijiuzulu kuinoa nchi hiyo baada ya kuenguliwa na Iceland katika michuano ya Ulaya iliyomalizika Jumapili iliyopita na toka wakati huo FA imekuwa ikisaka kocha atakayeziba nafasi yake. Sunderland wamethibitisha kuwa wamewaruhusu FA kufanya mazungumzo na Allardyce ambaye sasa ndio anatajwa kuwa kinara katika mbio hizo mbele ya Arsene Wenger na Jurgen Klinsmann ambao pia wanatajwa kutaka kupewa kibarua hicho. Sunderland ambao wamemaliza katika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu uliopita, nao pia wametaka mazungumzo na FA na wana matumaini wanaweza kuendelea kupata huduma ya Allardyce.
No comments:
Post a Comment