Friday, July 1, 2016

DEL BOSQUE AKUBALI YAISHE HISPANIA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amethibitisha kuwa ataachia wadhifa wake huo, siku chache baada ya mabingwa hao watetezi kung’olewa katika michuano ya Ulaya inayoendelea huko Ufaransa. Del Bosque mwenye umri wa miaka 65, mara kadhaa alishasema kuwa atajiuzulu nafasi hiyo kufuatia michuano hiyo na baada ya Hispania kupoteza mchezo wake wa hatua ya 16 bora dhidi ya Italia Jumatatu, amethibitisha kuwa ataondoka pindi mkataba wake utakapomalizika. Akihojiwa Del Bosque amesema bila kuwa na shaka yeyote hana nia ya kuendelea kubakia kuwa kocha hivyo baada ya michuano ya Ulaya ambapo ndio mkataba wake utamalizika ataondoka. Kocha wa zamani wa Granada Joaquin Caparros, kocha wa zamani wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Hispania, Julen Lopetegui na kocha wa zamani wan chi hiyo Jose Antonio Camacho wamekuwa watajwa kuchukua nafasi yake. Del Bosque ameingoza Hispania kutwaa taji la Kombe la Dunia mwaka 2010 na Euro 2012 lakini walitolewa katika hatua ya makundi katika Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment