MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesaini mkataba mpya wa miaka sita katika klabu hiyo yenye maskani yake Anfield. Klopp alijiunga na Liverpool Octoba mwaka jana, baadae akaja kukubali mkataba wenye thamani ya paundi milioni 15 ambao ulitarajiw akumalizika mwaka 2018 huku kukiwa na kipengele cha kuongezwa mwaka mwingine mmoja. Akihojiwa mara baada ya kusaini mkataba huo mpya, Klopp mwenye umri wa miaka 49, amesema amefurahi kwani ndio kwanza wameanza safari yao. Meneja huyo raia wa Ujerumani, aliisaidia Liverpool kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Ligi na Europa League msimu uliopita. Pamoja na kuwepo Anfield kwa kipindi cha miezi tisa pekee, kuongezwa mkataba kwa Klopp kunaonyesha jinsi gani viongozi walivyokuwa na imani naye.
No comments:
Post a Comment