TIMU ya NFL ya Dallas Cowboys ya Marekani imeipita klabu ya Real Madrid na kuongoza orodha ya timu zenye thamani zaidi duniani. Wakongwe hao wa La Liga na mabingwa wa Ulaya wamekuwa wakiongoza orodha hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, na Cowboys imekwea kileleni na kufanya kuwa timu ya kwanza ya NFL kukaa juu ya orodha hizo toka mwaka 2011. Hata hivyo, Madrid bado inabakia kuwa timu ya soka yenye thamani zaidi ikikadiriwa kuwa na thamani ya sola bilioni 3.65, ikiongoza orodha ya klabu nane za soka zilikuwepo katika orodha hiyo inayotolewa na jarida maarufu la Marekani la Forbes. Barcelona wao wako nyuma ya Madrid katika orodha hiyo wakikadiriw akuwa na thamani ya dola bilioni 3.55 huku Manchester United wakifuatia kwa kuwa na thamani ya dola bilioni 3.32, wakishika nafasi ya nane. Bayern mUnich wao wanashika nafasi ya 12 kwa kuwa na thamani ya dola bilioni 2.41, Arsenal nafasi ya 23 kwa kuwa na thamani ya dola bilioni 2.02, Manchester City nafasi ya 28 dola bilioni 1.92, Chelsea nafasi ya 36 dola bilioni 1.67 na Liverpool nafasi ya 41 dola bilioni 1.55.
No comments:
Post a Comment